Mwanamke akamatwa baada ya mtoto kufariki

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Polisi wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 37 baada ya kifo cha mtoto mchanga huko Birmingham nchini Uingereza

Mwanamke mwenye umri wa miaka 37 amekamatwa kwa tuhuma za kumtelekeza mtoto hadi kufa huko Birmingham.

Maafisa wa polisi waliitwa kwa ripoti kuhusu mtoto kisa cha mchanga mtoto anayehitaji dharura ya matibabu nyumbani kwao Culford Drive, Bartley Green

Polisi wa walisema mtoto huyo wa kiume alipelekwa hospitalini, ambapo kwa bahati mbaya alifariki.

“Tunaelewa wasiwasi wa jamii ya tukio hili, lakini tungeomba umma kutobashiri juu ya mazingira,” msemaji alisema.

Mwanamke huyo anaendelea kuzuiliwa na polisi kwa mahojiano.

Jirani mmoja aliiambia BBC kuwa kifo cha mtoto huyo kilikuwa “cha kuhuzunisha” na jambo ambalo hakuwahi kufikiria lingetokea kwa jirani yake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment