Mradi wenye utata wa kutengeneza DNA bandia ya binadamu waanza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Mradi wenye utata wa kutengeneza seli za msingi ambazo ni chanzo cha maisha ya binadamu umeanza kufanyiwa kazi katika kile kinachoaminika kuwa wa kwanza wa aina hii ulimwengu.

Utafiti wa mradi huo umekuwa mwiko hadi sasa kwa sababu ya wasiwasi kwamba unaweza kusababisha watoto waliotengenezwa kwa kubuniwa au kukawa na mabadiliko yasiyotarajiwa kwa vizazi vijavyo.

Lakini sasa shirika kubwa la kimatibabu duniani, Wellcome Trust, limetoa pauni milioni 10 za awali kuanza mradi huo na kuongeza kwamba una uwezekano wa kuwa chanzo cha mengi mazuri zaidi kuliko madhara kwa kuharakisha matibabu ya magonjwa mengi yasiyotibika.

Dk Julian Sale, wa Maabara ya MRC ya Biolojia ya Molekuli huko Cambridge, ambaye ni sehemu ya mradi huo, aliambia BBC kwamba utafiti huo utakuwa maendeleo makubwa yanayofuata katika biolojia.

“Hakuna kinachozuia mafanikio ya hili, tunaangalia tiba zitakazoboresha maisha ya watu kadri wanavyozeeka, zitakazochochea afya bora na magonjwa kidogo kadri wanavyozidi kuzeeka.

“Tunatazamia kutumia njia hii kuzalisha chembechembe zinazostahimili magonjwa tunazoweza kuzitumia kwenye viungo vilivyoharibika, kwa mfano kwenye ini na moyo, hata mfumo wa kinga mwilini,” alisema.

Lakini wakosoaji wanahofia kwamba utafiti huo utakuwa utatumiwa na watafiti wasio waaminifu kutafuta kutengeneza mwanadamu aliyeboreshwa zaidi au kubadilishwa.

Dk Pat Thomas, mkurugenzi wa kikundi cha kampeni cha Beyond GM, alisema: “Tunapenda kufikiria kwamba wanasayansi wote wapo kwa nia njema, lakini sayansi inaweza kutumika kwa nia tofauti kuleta madhara na katika vita”.

Maelezo ya mradi huo yalitolewa kwa BBC News katika kumbukumbu ya miaka 25 ya kukamilika kwa Mradi wa Jeni ya Binadamu, ambao ulipanga molekuli katika DNA ya binadamu na pia ulifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Wellcome.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment