Iran yathibitisha kifo cha kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,Ali Shadmani, mkuu wa kituo cha amri cha makao makuu ya IRGC ya Khatam al-Anbia.

Shirika la Habari la Fars limeripoti kuwa Ali Shadmani, mkuu wa kituo cha utoaji armi cha makao makuu ya kijeshi ya Khatam al-Anbia ya Iran, alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa makabiliano ya kijeshi na Israel.

Jeshi la Israel lilitangaza tarehe 17 Juni kuwa limemuua Shadmani, ambaye lilimtaja kuwa “mkuu wa majeshi wa Iran na kamanda wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi wa nchi hiyo.”

Meja Jenerali Gholam Ali Rashid aliwahi kuwa mkuu wa kituo cha amri cha makao makuu ya IRGC ya Khatam al-Anbia, lakini aliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga makamanda wakuu wa kijeshi wa Iran, maeneo ya nyuklia na wanasayansi mnamo Juni 13, usiku wa kwanza wa makabiliano ya kijeshi kati ya nchi hizo mbili .

Kiongozi Mkuu Ali Khamenei akamteua Ali Shadmani kama mrithi wa Gholam Rashid.

Mnamo Juni 17, Israel ilitangaza kumuua Shadmani, lakini Iran haikuthibitisha habari hizo wakati huo.

Makao Makuu ya Kati ya Khatam al-Anbia yanasimamia uratibu kati ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na vikosi vya kawaida vya kijeshi na hutumika kama kamandi kuu wakati wa vita, chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya Kiongozi Mkuu Ali Khamenei.

Iran itafanya mazishi ya kiserikali siku ya Alhamisi na Jumamosi kwa makamanda wakuu wa kijeshi, akiwemo Shadmani, na wanasayansi wakuu waliouawa wakati.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment