‘Hakutakuwa na vita tena Iran v Israel’-Trump

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais Donald Trump amesema Marekani itazungumza na Iran wiki ijayo na kwamba ‘hakutakuwa na vita tena kati ya Iran na Israel.’

Alipoulizwa nini kitatokea kwa Iran sasa hivi na ikiwa pengine ilihamishia nyenzo zake za nyuklia mahali pengine kabla ya shambulio la Marekani, Trump alijibu: “Hapana, hawakuwa na muda kabisa.” Aliongeza: “Nyenzo hii ni nzito sana na vigumu kuihamisha.”

Kulingana na yeye, uwezo wa nyuklia wa Iran sasa “umesambaratika.”

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio kisha akasema Rais Trump alikuwa tayari kuzungumza na wale wanaotaka amani na kuongeza kuwa mazungumzo hayo yanategemea iwapo Iran imedhamiria kufanya mazungumzo.

Trump alisema, “Tutazungumza na Iran wiki ijayo, labda tutafikia makubaliano.” Lakini pia alisema, “Mimi sihitaji makubaliano. Walipigana vita, sasa wanarudi kwenye ulimwengu wao wenyewe. Sijali kama kutakuwa na makubaliano au la.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment