Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Matatizo ya kimahusiano na makundi haya 5 ya watu.
ii. Matatizo ya kifedha
iii. Kuondokewa na mtu wa karibu mfano kuachwa au kufiwa.
iv. Kukabiliwa na Vitisho
v. Changamoto za ofisini
Katika Makala Hii Tutazungumzia Chanzo Cha Tano
– Changamoto za Ofisini
Kwenye eneo la kazi kuna mambo mawili, la kwanza ni mahusiano yako na bosi.
Kuna aina za mabosi ukiwa nao huwezi ukakwepa kupata msongo wa mawazo.
Hawa ni mabosi ambao ni kazi sana kuwaridhisha.
Hata ungefanya lolote bado hawawezi kufurahia. Kuna watu kila wakiamka asubuhi cha kwanza wanachowaza ni kelele za mabosi.
Akiona tu simu ya bosi inaingia, tayari ameshakuwa na msongo wa mawazo.
Pia kuna msongo wa mawazo unaosababishwa na wafanyakazi wenzako.
Ukipewa kazi pamoja nao unajuta kuwafahamu, ni wakorofi waliobobea.
Kwa hiyo kuna watu ambao wana msongo wa mawazo uliosababishwa na maeneo yao ya kazini.
Kilele cha msongo wa mawazo eneo la kazi ni pale ambapo unafukuzwa kazi tena bila kujiandaa kabisa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.