Mzozo wa Israel na Iran watatiza safari za ndege Mashariki ya Kati

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mashirika ya ndege yamefuta safari zake au kubadilisha njia za ndege kwenda na kutoka Mashariki ya Kati, huku mzozo kati ya Israel na Iran ukiendelea.

Uwanja wa ndege wa Doha nchini Qatar, ambao ni kitovu muhimu katika kanda hiyo, ulisitisha shughuli zake siku ya Jumatatu, baada ya Iran kurusha makombora katika kambi ya kijeshi ya Marekani nchini humo, kwa kile ilichosema ni kulipiza kisasi mashambulizi ya Marekani dhidi ya maeneo yake ya nyuklia mwishoni mwa juma.

Safari za ndege zilisitishwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Dubai huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kituo cha anga chenye shughuli nyingi zaidi duniani, huku abiria wakiambiwa watarajie kuchelewa na kufutwa zaidi kwa safari zao.

Zaidi ya mashirika 12 ya ndege yalifuta safari za kwenda sehemu za eneo hilo baada ya mvutano kuongezeka katika siku za hivi majuzi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment