Trump asherehekea kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika ujumbe kwenye jukwaa la mawasiliano la Truth Social akisema Marekani ilisababisha “uharibifu mkubwa” katika mashambulizi iliyotekeleza kwenye “maeneo yote ya nyuklia nchini Iran”.

“’Obliteration’ ndio neno sahihi,” aliandika kwenye ujumbe huo akimaanisha uharibifu kabisa.

Akirejelea picha ya satelaiti ambayo hakuishirikisha katika ujumbe wake, Trump alisema “muundo mweupe ulioonyeshwa upo chini ya mwamba” na “umelindwa dhidi ya moto”, wakati “uharibifu mkubwa ulifanyika chini ardhi kabisa.”

“Bullseye!!!” aliongeza neno hilo mwishoni mwa ujumbe wake akimaanisha mahali sahihi palipolengwa.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema mashambulizi hayo ni “hatari” kwani yanaweza kutanuka katika maeneo mengine kwa “haraka” mno huku shirika lake la uangalizi wa nyuklia likisema kuwa halijaweza kutathmini ipasavyo uharibifu uliofanywa.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment