Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Jeshi la Colombia limesema wanajeshi 57 wametekwa nyara na raia katika eneo la Micay Canyon kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Jeshi limesema wanajeshi 31 walitekwa siku ya Jumamosi huku waliosalia wakitekwa nyara siku ya Jumapili na kundi la zaidi ya watu 200.
Jeshi linasema kuwa raia hao wako chini ya shinikizo kutoka kwa waasi wa kundi la Farc ambalo lilikubali mapatano ya amani na serikali mwaka 2016.
Eneo la milimani linatumika kwa kiasi kikubwa kwenye uzalishaji wa kokeini na linasalia kuwa moja ya yalio katika mzozo unaoendelea nchini humo na makundi ya waasi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.