Maelfu ya Waislaeli waachwa bila umeme kufuatia mashambulizi ya Iran – waziri

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baadhi ya Waisraeli wanakimbilia katika makazi salama ya chini ya ardhi mjini Tel Aviv mnamo Juni 23
Maelezo ya picha,Baadhi ya Waisraeli wanakimbilia katika makazi salama ya chini ya ardhi mjini Tel Aviv mnamo Juni 23

Takriban watu 8,000 nchini Israel hawana umeme kufuatia mashambulizi ya makombora Iran asubuhi ya leo, kulingana na waziri wa Kawi wa nchi hiyo.

Eli Cohen anasema mamlaka ilikuwa “imejiandaa kukabiliana na uharibifu wa miundombinu ya umeme” na inajiatahidi kurejesha kuwarejeshea wakazi umeme ndani ya saa tatu.

Shirika Umeme la Israel (IEC) awalili liliripoti “kuharibiwa kwa miundombinu wa kituo cha kimkakati” eneo la kusini, na kusababisha kukatizwa kwa huduma za umeme kwa wakazi kadhaa.

“Wahudumu wa IEC wanaelekea katika maeneo tofauti kurekebisha hitilafu zilizosababisha kupotea kwa umeme haraka iwezekanavyo. Operesheni hizo ni pamoja na ukarabati wa miundombinu na kupunguza hatari za usalama, na zinafanywa kwa uratibu na vikosi vya usalama, “inasema.

Operesheni hizo ni pamoja na ukarabati wa miundombinu na kupunguza hatari za usalama, na zinafanywa kwa uratibu na vikosi vya usalama, “inasema.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment