Liverpool inakaribia kumalizana na Milos Kerkez wa Bournemouth

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

s

Klabu ya Liverpool imekaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 40 kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto wa Bournemouth, Milos Kerkez. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anaelezwa kuwa na hamu Kuba ya kujiunga na Liverpool, na masharti binafsi hayatarajiwi kuwa kikwazo.

Liverpool imekuwa na imani kubwa kuhusu kumsajili beki huyo wa kushoto ambaye alijiunga na Bournemouth msimu wa joto wa mwaka 2023 akitokea AZ Alkmaar.

Kerkez anatarajiwa kuwa usajili wa hivi karibuni wa Arne Slot katika dirisha hili la usajili, baada ya tayari kumchukua Jeremie Frimpong kwa mkataba wa pauni milioni 29.5 kutoka Bayer Leverkusen, huku Florian Wirtz pia akikaribia kuhamia kwa pauni milioni 116.5 kutoka klabu hiyo hiyo.

Kerkez amekuwa mmoja wa wachezaji bora wa Bournemouth, akifunga mabao mawili na kutoa pasi tano za mabao katika mechi 38 za Ligi Kuu msimu uliopita, na Liverpool wamekuwa wakimwania kwa muda mrefu.

Mkurugenzi wa Michezo wa Liverpool, Richard Hughes ambaye alijiunga na klabu hiyo kutoka Bournemouth msimu wa joto uliopita ndiye aliyemsajili Kerkez awali kwenda Bournemouth akitokea AZ Alkmaar mwaka 2023.

Mapema wiki hii, Bournemouth ilikamilisha dili la kumsajili beki wa kushoto Adrien Truffert kutoka Rennes. Truffert, ambaye alijiunga na Bournemouth kwa mkataba wa awali wa pauni milioni 10.1 unaoweza kuongezeka hadi pauni milioni 14.3, anaonekana kama mbadala wa Kerkez.

Florian Wirtz akamilisha vipimo vya afya Liverpool

s

Florian Wirtz amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Liverpool Ijumaa asubuhi kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 100 kwenda kwa mabingwa wa Ligi Kuu.

Uhamisho unavunyja rekodi ya awali ya pauni milioni 115 iliyolipwa na Chelsea kwa ajili ya Moises Caicedo.

Sky huko Ujerumani inaripoti kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amefanikiwa kukamilisha sehemu ya kwanza ya vipimo vyake vya afya. Aliwasili Uingereza Alhamisi.

Sehemu ya pili ya vipimo itafanyika jioni hii, baada ya hapo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na mshahara wa chini wa pauni 195,000 kwa wiki, ambao unaweza kufikia pauni 245,000 kwa wiki ukijumlisha nyongeza za bonasi.

“Huu ni usajili mkubwa kutoka kwa mabingwa,” aliripoti Ben Ransom wa Sky Sports News kutoka nje ya uwanja wa mazoezi wa Liverpool Ijumaa asubuhi. “Tunatarajia kutangazwa wakati wowote kuanzia.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment