Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Marekani kuingilia kati mzozo kati ya Israel na Iran kutasababisha “hali kuwa mbaya zaidi”, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov ameliambia shirika la habari la serikali ya Urusi TASS.
Marekani na Urusi zinaunga mkono pande tofauti katika mzozo huo.
Wakati Donald Trump anadai Iran “kujisalimisha bila masharti” na anaripotiwa kuwa anafikiria kuishambulia, Moscow inaiona Tehran kama mshirika mkuu.
Mapema mwaka huu, Vladimir Putin alitia saini mkataba wa kina wa ushirikiano wa kimkakati na mwenzake wa Iran, Masoud Pezeshkian, Kifungu cha Kwanza mkataba wao kikisema wana nia ya kuendeleza ushirikiano wa ulinzi na usalama.
Iran pia imeipatia Urusi ndege zisizo na rubani za Shahed ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imelaani mashambulizi ya Israel na kusema ni “ya kijinga” ambayo “hayachochewa na chochote”, na hapo jana naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov aliionya Marekani kutotoa msaada wa kijeshi kwa Israel.
“Hii inaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi,” alisema.
Haya yote yanaiweka Moscow na Washington kwenye hali tete katika mgogoro wa Israel na Iran, na inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika uhusiano wa Urusi na Marekani ambao umekuwa ukiimarika tangu kuchaguliwa tena kwa Donald Trump.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.