Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Televisheni ya taifa ya Iran imewatahadharisha watumiaji kuhusu video “isiyo na maana” inayoutolea wito umma “kuasi” dhidi ya serikali, ambayo iliripotiwa kuonekana kwenye chaneli zake za satelaiti.
“Ukiona ujumbe wowote usio na maana unapotazama TV, ni kwasababu adui anaziba ishara za satelaiti,” taarifa ya televisheni ya serikali ilisema.
Video hiyo, ambayo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, ilishutumu taifa la Iran kwa “kushindwa kuwahudumia” watu wake na kuwataka watazamaji “kuchukua udhibiti wa maisha yao ya baadaye.”
Chanzo cha video hii au udukuzi wa televisheni ya serikali bado hakijajulikana.
Nembo ya simba ilionekana kwenye kona ya juu kulia ya video. Video hiyo pia ilikuwa na picha za viongozi wakuu wa Iran waliouawa na Israel wakati wa shambulizi dhidi ya Iran,- katika operesheni inayojulikana kwenye vyombo vya habari kama “Operesheni Rising Lion,” mnamo Juni 13.
Video hiyo pia ilikuwa na picha za maandamano makubwa yaliyofanyika nchini Iran mwaka 2022, yaliyochochewa na mauaji ya Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi kwa madai ya kushindwa kuzingatia sheria za hijab.
Kauli mbiu ya maandamano hayo ilikuwa “Wanawake, Maisha, Uhuru,” msemo uliotumiwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye, kama inavyoonekana kwenye video hiyo, aliwataka Wairani kuanzisha “maasi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.