Netanyahu anachezea ‘hisia za kutojiamini’ za Trump, mshauri wake wa zamani asema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakati ulimwengu ukisubiri uamuzi wa Trump kuhusu shambulizi la Marekani, Anthony Scaramucci mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano wa Ikulu ya White House aliyehudumu katika muhula wa kwanza wa Trump, ameelezea mchakato wa kufanya maamuzi wa rais wa Marekani.

“Hakuna mshikamano, hakuna sera ya msingi … ni sera za kuruka bila kufikiria kimkakati,” anaiambia BBC Newsnight.

Scaramucci anaongeza kuwa anadhani Benjamin Netanyahu amecheza na “hisia za kutojiamini za Trump kuhusu namna anavyotaka kuonekana mbabe” kujaribu kumshawishi ajiunge na mzozo.

Akizungumzia uwezekano wa Marekani kuhusika katika mabadiliko ya utawala nchini Iran, anasema: “Hatujajifunza chochote katika miongo miwili… Sio wazi kwangu Wamarekani wanapaswa kuwa ndio wanaosukuma mabadiliko ya utawala.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment