Kiongozi wa Iran ‘hapaswi kuendelea kuwepo’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, “hapaswi kuendelea kuwepo” baada ya hospitali ya Soroka kushambuliwa na kombora la Iran, kulingana na vyombo vya habari vya ndani na shirika la habari la AFP.

Akiongea na waandishi wa habari huko Holon, karibu na Tel Aviv, Israel Katz aliripotiwa kusema: “Khamenei ametangaza wazi kwamba anataka Israel iangamizwe, yeye binafsi ametoa agizo la kufyatua risasi hospitalini.

“Anachukulia kuangamizwa kwa taifa la Israeli kuwa lengo lake…Mtu wa namna hii hapaswi kuendelea kuwepo.”

Hata hivyo waziri Katz, hajaweka bayana kwamba hapaswi kuwepo kwa maana ya kuondolewa mamlakani ama kuuawa.

Hapo awali, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vilisema lengo kuu la shambulio la kombora la asubuhi ya leo lilikuwa eneo la kijeshi karibu na Hospitali ya Soroka, sio hospitali yenyewe.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment