Iran na Israel zafanya mashambulizi zaidi huku Trump akipima uingiliaji kati wa Marekani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne usiku aliidhinisha mipango ya kushambulia Iran, lakini hajafanya uamuzi wa mwisho kuhusu kuishambulia nchi hiyo, shirika la BBC la Marekani CBS linaripoti.

Trump ataacha kuanzisha mashambulizi ikiwa Iran itakubali kuachana na mpango wake wa nyuklia, chanzo kikuu cha ujasusi wa Marekani kiliiambia CBS.

Habari hiyo iliripotiwa kwa mara ya kwanza na Wall Street Journal.

Siku ya Jumatano, Trump alisema, “Naweza au siwezi kuyafanya”, alipoulizwa swali kuhusu ushiriki wa Marekani nchini Iran.

Trump anayapima mashambulizi ya Marekani dhidi ya Fordo, kituo cha kurutubisha urani chini ya ardhi nchini Iran, CBS iliripoti mapema.

Haya yanajiri huku jeshi la anga la Israeli linasema limenasa ndege isiyo na rubani kutoka Iran baada ya tahadhari kutolewa mapema Alhamisi asubuhi.

“Jeshi la anga lilinasa ndege isiyo na rubani iliyopaa kutoka Iran,” iliandika kwenye X.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vinasema vimepiga zaidi ya malengo 20 ya kijeshi katika mji mkuu wa Iran.

Iimesema limeyapiga “maeneo muhimu ya nyuklia na makombora” huko Tehran ambayo linasema ni maeneo ”yanayochochea mpango wa silaha wa Iran na mashambulizi dhidi ya raia wa Israeli”.

Mifumo ya ulinzi ya Israeli inakatiza makombora mengi yanayorushwa kuelekea humo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment