Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Moja ya injini za ndege ya Air India iliyoanguka wiki iliyopita ilikuwa mpya, wakati nyingine ilipaswa kufanya kazi hadi Desemba, mwenyekiti wa shirika hilo alisema.
Katika mahojiano na kituo cha habari cha India, N Chandrasekaran alisema kuwa injini zote mbili za ndege hiyo zilikuwa “sawa”.
“Injini ya kulia ilikuwa injini mpya iliyowekwa Machi 2025. Injini ya kushoto ilfanyiwa huduma ya kawaida mara ya mwisho mnamo 2023 na ilitarajiwa kuangaliwa upya mnamo Desemba 2025,” aliambia kituo cha Times Now.
Takriban watu 270, wengi wao wakiwa abiria, waliuawa Alhamisi iliyopita wakati AI171, ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyokuwa ikielekea London, ilipoanguka chini ya dakika moja baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad magharibi mwa India.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.