Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais Donald Trump amefanua mkutano wa dharura katika Ikulu ya White House. Mkutano huo, uliochukua saa moja na dakika ishirini, ulifanyika ili kujadili iwapo Marekani inapaswa kuungana na Israel kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran, Shirika la habari la Marekani na washirika wetu cha CBS News kimeripoti.
Ripoti hiyo inasema hakuna makubaliano kamili kati ya washauri wa karibu wa Bw Trump.
Baada ya siku kadhaa kuwataka Wairani kurejea kwenye mazungumzo, Rais Trump anatafakari iwapo Marekani inapaswa kuhusika moja kwa moja katika vita vya Israel dhidi ya Iran.
Katika mkutano wa Jumanne wa baraza la usalama la taifa la Marekani, Bw Trump na washauri wake wanaripotiwa kujadili uwezekano wa kushambulia maeneo ya nyuklia ya Iran.
Lengo moja linalowezekana linaweza kuwa eneo la kurutubisha madini ya uranium huko Fordo lililopo chini ya ardhi.
Ni Wamarekani pekee ndio wenye bomu lenye uwezo wa kuliangamiza. Kulingana na CBS News, washauri wa rais bado wamegawanyika kuhusu jinsi ya kulitekeleza hili.
Vyombo vya habari vya Marekani na Israel vinasema kuwa baada ya mkutano huo Bw Trump alimpigia simu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, lakini haijajulikana kilichojadiliwa.
Katika muda wa siku tatu zilizopita, angalau ndege 30 za kijeshi za Marekani – zinazotumiwa kujaza mafuta kwa ndege za kivita na mabomu – zimesafirishwa hadi Ulaya.
Jana, katika msururu wa machapisho kwenye mitandao ya kijamii, Bw Trump aliitaka Iran ijisalimishe bila masharti.
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alijibu kwa msururu wa jumbe zake za mitandao ya kijamii jana usiku – akisisitiza kuwa nchi yake “haitakubali kamwe maelewano na Wazayuni.”
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.