Mjue Aina Ya Bosi Uliyenaye, Ili Asiwe Kikwazo Katika Kutimiza Ndoto Zako…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Bosi Anayetaka kusimamia kila kitu (Micromanager).
ii. Bosi ambaye hapatikani
iii. Bosi asiye na uwezo (Incompetent Boss).
iv. Bosi anayekuchukua bila sababu za msingi (Bigot Boss)
v. Bosi mjuaji wa kila kitu na mtumia mabavu (Despot Boss).

Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina Ya Kwanza

– Bosi Anayetaka kusimamia kila kitu (Micromanager).

Unaweza kupata kazi nzuri unayoipenda ila ukipata bosi wa hivi unatakiwa kujua namna ya kudeal naye kwani anaweza kukusababishia “stress” (msongo wa mawazo) za hali ya juu.

Bosi wa namna hii anapenda kusimamia kila kitu bila kujali ni kidogo kiasi gani.

Hata ikitokea anakuagiza kununua chakula atakupa maelekezo kama vile ndio mara yako ya kwanza kununua.

Akikupa kazi huwa hakupi nafasi ya kutumia ubunifu, kila saa yuko shingoni kwako kukufuatilia unavyotekeleza kazi zako.

Mara nyingi ukifanya kazi na mtu wa namna hii unaweza kujiona kama vile huwezi kazi kwa sababu mabosi wa hivi wengi huwa wanaona wao ndio wanajua zaidi ya kila mtu.

Madhara yao makubwa ni kuwa wanapenda kukosoa sana kwa sababu wao hudhani wao ni bora kuliko mtu yoyote na wanaamini njia zao za kufanya kitu ndio sahihi.

Huwa hawakupi nafasi ya kutumia ubunifu hata kidogo.

Ukiwa naye wa namna hii inabidi kazi zako uzifanye kwa kasi sana kabla ya muda uliotarajiwa ili uepuke kuulizwa ulizwa kila wakati na jitahidi kabla ya muda unaotakiwa uwe umemaliza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment