Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Genge moja limezuia kwa muda maandamano ya kutaka Naibu Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya Eliud Lagat ajiuzulu.
Waandamanaji wanaopinga Lagat waliokuwa wakiandamana katikati ya Nairobi walilazimika kukimbia ili kujilinda huku magenge ya bodaboda yaliokuwa yakipinga maandamano hayo yalipowakabili.
Wapinzani hao ambao walifika kwa kishindo kwa pikipiki kadhaa waliwazuia waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi kwenye makutano ya barabara ya University Way na kutatiza maandamano hayo.
Waandamanaji dhidi ya Lagat walilazimika kutoroka huku wapinzani wao wakichukua udhibiti kwa muda.
Wakati huo wote magari ya polisi na maafisa walionekana wakishuhudia jinsi magenge hayo yalivyokuwa yakiwakimbiza na kuwapigia kelele waandamanaji.
Hapo awali, polisi walikuwa wametumia vitoa machozi kutawanya umati uliokuwa umekusanyika katika Kituo cha habari cha Nation ambapo ghadhabu ilianza.
Mvutano huo umelemaza shughuli za biashara ndani ya mji na maduka tayari yamefungwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.