Takriban watu 45 wauawa karibu na eneo la kutoa misaada Gaza – Hamas

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Makumi ya Wapalestina zaidi wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika kisa cha hivi punde karibu na eneo la kusambaza misaada huko Gaza.

Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema kuwa watu 45 wameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel. Hospitali kuu inayofanya kazi katika eneo hilo inazidiwa na idadi ya majeruhi.

BBC imeomba Wanajeshi wa Ulinzi wa Israel kutoa maoni yao.

Hili linaweza kuwa tukio baya zaidi kufikia sasa katika ufyatuaji wa risasi karibu kila siku ambao unafanyika karibu na maeneo ya usambazaji wa misaada huko Gaza.

Walioshuhudia wanasema kuwa wanajeshi wa Israel walifyatua risasi na kushambulia kwa makombora eneo karibu na makutano ya mashariki mwa mji wa kusini wa Khan Younis ambapo maelfu ya Wapalestina walikuwa wamekusanyika kwa matumaini ya kupokea chakula.

Katika hospitali ya Nasser, kuna msongamano mkubwa kiasi kwamba majeruhi wengi wamelala chini huku wahudumu wa afya wakiwatibu majeraha yao.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment