‘Kila mtu anapaswa kuondoka mara moja Tehran’, anasema Trump

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Trump

Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth, Rais wa Marekani Donald Trump anasema kwamba “kila mtu anapaswa kuondoka mara moja Tehran”.

Kauli yake inakuja baada ya maafisa wa Israel kuwashauri wakazi kuhama maeneo ya kaskazini mashariki mwa Tehran mapema leo, wakisema kuwa inapanga kulenga “miundombinu ya kijeshi”.

Trump anaongeza kuwa Iran ilipaswa kutia saini makubaliano ambayo aliweka mbele yao katika duru ya hivi karibuni zaidi ya mazungumzo ya nyuklia ya Marekani na Iran.

“Kwa kifupi, IRAN HAIWEZI KUWA NA SILAHA YA nyuklia,” anaandika. “Nilisema tena na tena!

“Kila mtu anapaswa kuondoka mara moja Tehran!”

Mwandishi wa BBC Anthony Zurcher yuko Alberta, Canada, katika mkutano wa G7, ambao Trump anahudhuria. Mwanahabari wetu alimuuliza msaidizi wa rais wa vyombo vya habari kwa ajili ya ufafanuzi kwenye chapisho lake la mtandao wa kijamii.

Zurcher aliagizwa kuwasiliana na timu kuu ya waandishi wa habari wa White House huko Washington kwaajili ya maoni. Endelea kuwa nasi tunapofuatilia hili.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment