‘Tuko njiani kupata ushindi’ – Netanyahu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

,

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema “tuko njiani kupata ushindi”.

Akitembelea kambi ya anga ya Israel, alirejelea madai ambayo tumesikia kutoka Israel leo – kwamba “inadhibiti anga ya Tehran”.

“Tuko njiani kufikia malengo yetu mawili: kuondoa tishio la nyuklia na kukomesha tishio la makombora,” alisema.

Netanyahu pia alisema anataka kuleta tofauti kati ya mashambulizi ya Israel na yale ya Iran, akiongeza kuwa haya ndiyo malengo ya Israel na kudai Iran inalenga raia.

“Tunawaambia raia wa Tehran: ‘Ondokeni’ – na tutachukua hatua,” alisema.

Aliwaambia wale wanaofanya kazi kwenye kituo cha kambi za jeshi: “Asanteni, na kwa uwezo wa Mungu – tutachukua hatua na kufanikiwa, na kuendelea hadi tupate ushindi.”

Wizara ya afya ya Iran imeripoti kuwa takriban watu 224 wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu Ijumaa.

Hata hivyo, waandishi wa habari wa BBC hawawezi kuripoti kutoka ndani ya Iran kutokana na vikwazo vya serikali ya nchi hiyo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment