Televisheni ya taifa ya Iran yasema imeshambuliwa na Israel

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Iran News Network, ambao ni sehemu ya kituo cha televisheni cha taifa cha Iran, imesema kuwa imeshambuliwa na Israel, kulingana na ripoti za Reuters.

Hii inafuatia vitisho vya awali kutoka kwa waziri wa ulinzi wa Israel, ambaye alisema shirika la utangazaji la serikali lilikuwa “linakaribia kutoweka”.

Muda mfupi baadaye, ilifanikiwa kurejelea matangazo yake ya moja kwa moja.

Mtangazaji alisema kwamba vipindi vyake vyote “vinaanza tena kupeperushwa moja kwa moja bila kukatizwa”.

Mtangazaji huyo alisema kuwa Israel ilikuwa ikijaribu “kunyamazisha sauti ya ukweli” kwa kuishambulia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment