Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bei ya mafuta duniani imepanda baada ya Israel kusema kuwa imeishambulia Iran, katika hali ambayo huenda ikaibua mvutano mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati.
Bei ya mafuta ghafi ya Brent ilipanda kwa zaidi ya 10% muda mfupi baada ya taarifa za shambulio hilo kuibuka, na kufikia kiwango chake cha juu tangu mwezi Januari.
Wafanyabiashara wana wasiwasi kuwa mzozo kati ya Iran na Israel unaweza kutatiza usambazaji wa mafuta kutoka eneo hilo lenye utajiri wa nishati.
Gharama ya mafuta ambayo hayajasafishwa huathiri kila kitu kuanzia gharama ya kuweka gari lako mafuta hadi bei ya chakula madukani.
Baada ya bei ya mafuta ghafi ya Brent crude ilipanda kwa 8% kuliko ilivyokuwa Alhamisi, na kufanya bei kufikia takriban $74.65 kwa pipa
Licha ya matukio ya hivi pundi, bei ya mafuta bado iko chini zaidi ya 10% kuliko ilivyokuwa katika kiwango sawa na hicho mwaka jana.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.