Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Makumi ya Wapalestina wameuawa walipokuwa wakijaribu kufikia msaada huko Gaza, hospitali zilisema.
Hospitali mbili katika jiji la Gaza zilisema watu 25 waliuawa usiku kucha, karibu na msafara wa kusafirisha unga na eneo la usambazaji wa chakula linaloendeshwa na Wakfu wa kutoa misaada ya Kibinadamu huko Gaza (GHF) unaoungwa mkono na Marekani na Israel katika eneo la ukanda wa Netzarim.
Shirika la Ulinzi la Raia linaloendeshwa na Hamas limesema kuwa vikosi vya Israel vilifyatua risasi. Pia kuna taarifa za watu kukandamizwa na lori na kupigwa risasi na Wapalestina.
Jeshi la Israel limesema wanajeshi walifyatua risasi za onyo huku washukiwa wakiwakaribia.
Tukio la Israel la ufyatuaji risasi liliwaua watu wengine 14 karibu na eneo la GHF huko Rafah kusini mwaka Gaza, hospitali ya Khan Younis ilisema.
Jeshi la Israel lilisema lilikuwa likichunguza ripoti hizo kutoka Rafah.
GHF ilisema zaidi ya vifungashio 43,000 vya chakula vilikabidhiwa vituo vyake vitatu vya usambazaji huko Rafah na Gaza ya kati “bila kushuhudiwa matukio kama hayo” siku ya Jumatano.
Hata hivyo, kumekuwa na matukio mabaya karibu na maeneo ya GHF karibu kila siku tangu mfumo wake wa usaidizi wenye utata ulipoanza kufanya kazi tarehe 26 Mei.
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema watu 223 wameuawa walipokuwa wakijaribu kufikia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya usambazaji wa misaada katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, wakiwemo 57 siku ya Jumatano.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.