Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mamia ya maelfu ya watu wanaendelea kukabiliwa na “njaa” katika kambi za wakimbizi za Kenya baada ya kupunguzwa kwa ufadhili wa Marekani kusababisha kupungua kwa mgao wa chakula hadi viwango vya chini kuwahi kutokea, afisa wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.
Athari hiyo inaonekana wazi katika hospitali iliyo kwenye kambi ya Kakuma kaskazini-magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Ni nyumbani kwa takriban wakimbizi 300,000 ambao wamekimbia mapigano katika nchi za barani Afrika na Mashariki ya Kati.
Watoto waliodhoofika wamejaa katika wodi ya vitanda 30 kwenye Hospitali ya Amusait ya Kakuma, wakiwatazama wageni huku wakiwa wanapokea matibabu kwa utapiamlo mbaya.
Mtoto mmoja, Hellen, anashindwa kutembea. Sehemu za ngozi yake imekunjana na kuchubuka, na kuacha mabaka mekundu – matokeo ya utapiamlo, daktari aliambia BBC.
Mtoto mchanga wa miezi tisa, James, wa nane wa Agnes Awila, mkimbizi kutoka kaskazini mwa Uganda.
“Chakula hakitoshi, watoto wangu wanakula mara moja tu kwa siku. Ikiwa hakuna chakula utawalisha nini?” anauliza.
James, Hellen na maelfu ya wakimbizi wengine huko Kakuma wanategemea Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kupata riziki.
Lakini shirika hilo lililazimika kupunguza kwa kiasi kikubwa shughuli zake katika nchi nyingi baada ya Rais Donald Trump kutangaza kupunguza kwa kiasi kikubwa misaada yake kwa nchi za kigeni mapema mwaka huu, kama sehemu ya sera yake ya “Marekani Kwanza”.
Marekani ilikuwa imetoa takriban 70% ya fedha kwa ajili ya shughuli za WFP nchini Kenya.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.