Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Afisa wa zamani wa CIA ambaye alifichua nyaraka za siri kuhusu mipango ya Israel kuishambulia Iran amehukumiwa kifungo cha miezi 37 jela.
Mwezi Januari, Asif William Rahman, 34, alikiri kutekeleza makosa mawili ya kuhifadhi kimakusudi na kusambaza taarifa za ulinzi wa taifa chini ya Sheria ya Ujasusi.
Mamlaka zinasema kwamba, kwa kutumia kibali chake cha ngazi ya juu cha usalama, Rahman alichapisha, kupiga picha na kutuma nyaraka zenye siri kubwa. Baadaye ziliishia kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Israel ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran Oktoba mwaka jana, ikilenga maeneo ya kijeshi katika mikoa kadhaa, ili kukabiliana na msururu wa makombora yaliyorushwa na Tehran wiki zilizokuwa zimetangulia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.