Mzozo wa mazishi ya aliyekuwa rais wa Zambia wachanganya waombolezaji

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Kupanga mazishi kunaweza kuwa majaribio makubwa hali ikiwa sio tofauti hata kwa rais wa zamani nchini Zambia.

Watu wakiwa katika hali ya huzuni, wapendwa lazima wafikirie kuhusu gharama, matakwa ya mwendazake na mambo mengine mengi ili kumuaga mpendwa wenu kwa njia ambayo mungependa.

Kwa kiongozi huyu wa zamani, jumuisha matakwa ya serikali, wapinzani wa kisiasa na familia hali inaweza kuwa ngumu mara mbili.

Edgar Lungu, ambaye aliongoza Zambia kutoka mwaka 2015 hadi 2021, alifariki Alhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 68.

Kifo chake kimewashtua Wazambia – na kuna hali ya huzuni ya kweli huku vituo vyote vya redio vikipiga muziki wa injili kwa kiongozi huyo ambaye alikuwa amebakia kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Zambia licha ya kuzuiwa kugombea uchaguzi wa mwaka jana.

Zambia ni rasmi nchi ya Kikristo – na watu wengi huchukulia dini na vipindi vyao vya maombolezo kwa umuhimu mkubwa.

Lakini mvutano kati ya familia yake, serikali na chama cha siasa cha Lungu, Patriotic Front (PF), umewaacha waombolezaji wakiwa wamechanganyikiwa kuhusu jinsi gani hasa rais huyo wa zamani anapaswa kupewa heshima yake ya mwisho.

Serikali ilitangaza kutakuwa na mazishi ya kitaifa na kutangaza kwamba mahali rasmi pa maombolezo itakuwa sehemu ya kulala wageni inayomiliki katika mji mkuu, Lusaka, lakini chama cha PF kilitupilia mbali mpango huu, na badala yake, kikaelekeza waombolezaji kwenye makao yake makuu.

Kuhusu familia ya Lungu, wamesema hawapingi mazishi ya serikali, lakini wamesisitiza kuchagua ni nani atakayesimamia mazishi hayo, wakili wa familia Makebi Zulu ameambia BBC.

Kisha kuna kitabu rasmi cha maombolezo, ambacho waombolezaji wanaweza kumuenzi Lungu. Serikali imetenga kitabu rasmi – katika eneo walilolitenga – lakini PF imewataka watu kusaini kitabu chao – katika makao yao makuu.

Serikali ilitaka kurudisha mwili wake kutoka Afrika Kusini wiki iliyopita – Lungu alifia huko baada ya kupata matibabu ya ugonjwa ambao haukujulikana.

Hata hivyo, PF na familia ya Lungu waliingilia kati, wakitaka kupewe fursa ya kufanya maandalizi wanayotaka kwa kiongozi huyo wa zamani.

“Serikali ilikuwa ikisema, ‘Tunampa heshima kamili ya kijeshi, kwa hivyo tutachukua mwili kuanzia hapa’ – kana kwamba wanasema ‘hamna uamuzi juu ya kile kinachotokea,'” Bw Zulu alisema.

Mipango ya kurejesha mwili wa Lungu bado haijulikani, ingawa familia sasa inashirikiana na serikali kuhusu suala hili.

Pia kumekuwa na mkanganyiko juu ya kipindi “rasmi” cha maombolezo wakati aina zote za burudani kama vile mechi kubwa za kandanda na matamasha zimesimamishwa.

Serikali ilitangaza kipindi cha siku saba cha maombolezo ya kitaifa kuanzia Jumamosi iliyopita, ingawa PF ilitangaza siku moja kabla.

Mkanganyiko huu, unaonekana kuwa mwendelezo wa uhusiano wa misukosuko kati ya Lungu na mrithi wake, Rais Hakainde Hichilema.

Wawili hao ni wapinzani wa muda mrefu – mnamo 2017, Lungu alipokuwa rais, Hichilema aliwekwa kizuizini kwa zaidi ya siku 100 kwa tuhuma za uhaini baada ya msafara wa Hichilema kudaiwa kukataa kumpisha njia.

Ilibidi Jumuiya ya Madola kuingilia kati kwa Hichilema kuachiliwa. Miaka minne baadaye, na baada ya majaribio matano ya urais, Hichilema alimshinda Lungu.

Sasa, chama cha PF na wakili wa familia ya Lungu wanaishutumu serikali ya Hichilema kwa kuhusika kwa kiasi fulani na kifo cha rais huyo wa zamani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment