Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

1.Pombe.
Pombe imeharibu hatima za vijana wengi hasa kwa kufuja pesa.
Wengi wamefukuzwa kazi kwasababu ya ulevi.
Pombe nyingi ni gharama.
Kunywa pombe nyingi kunakausha mifuko.
2.Wanawake.
Wanawake ni mama zetu.
Wanawake ni Dada zetu.
Bahati mbaya kuna viumbe vimefanya kiumbe huyu tumuone hatari sana.
Vijana wengi hatima zao zinafia kwenye mapaja ya Wanawake.
Pesa nyingi zinaishia kwenye mapaja ya Wanawake.
OK.
Ni starehe yako lakini haina shida.
3.Kubeti.
Watu wanabeti kiasi cha kusahau ndoto zao.
Wengi wanaamini betting itatimiza ndoto zao.
Ukweli ni kwamba baadhi yenu betting itachukua hata hicho kidogo mlichonacho.
Ingia shambani
Uza nyanya.
Uza bagia.
Betting itakuletea pesa ukibahatisha ila haiwezi kukufanya tajiri.
Betting will bring you money but will not make you rich.
Kimbia .
4.Ukosefu wa Elimu ya fedha.
Hii elimu ndiyo inayoongoza Dunia.
Hii elimu haifundishwi kwenye mitaala ya shule.
Sijui kwanini lakini Educational stakeholders wanaweza kutwambia.
Wengi wanafanya manunuzi ya hovyo.
Mtu ananunua simu ya laki nne mwezi ujao anauza laki na hamsini.
Wewe siyo mjanja ni mjinga.
Jifunze Fedha zinavyofanya kazi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.