Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ii. Mahusiano Na Familia
iii. Vifo Kabla Ya Wakati
iv. Kukataliwa
v. Fedha Na Uchumi
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Pili
– Mahusiano Na Familia
Mstari huu kwenye familia huwa unahusisha changamoto zisizoisha kwenye mahusiano.
Ukiiangalia familia ya namna hii wanaweza kuwa wamesoma au wana pesa lakini kwenye eneo la mahusiano kunakuwa na vurugu za kila aina na huwasababishia watu wa familia hiyo wasifurahie kabisa maisha yao.
Katika familia za namna hii ni kawaida sana kukuta watu wana watoto wa nje, unakuta karibu kila mwanaume ana mtoto wa nje na imekuwa ni jambo la kawaida.
Watu kuzaa kabla ya kufunga ndoa sio jambo la kushangaza kabisa, na huwa halishtui pale linapotokea.
Kunakuwa na wasichana wengi ambao unakuta wanazaa wakiwa bado wanafunzi au wakiwa na umri mdogo sana.
Si ajabu kabisa kwenye familia za namna hii, kukuta wanawake wakiwa na umri mkubwa ila wanataka kuolewa na mahusiano yao huwa yanaishia njiani.
Unakuta wapo wengi sana waliosoma vizuri, wana kazi nzuri au wanabiashara zao nzuri, ila huwa hawafanikiwi kabisa kupata wenza wa maisha yao.
Unakuta kuna wanawake wengi watu wazima kwenye familia hizi ila hawako kwenye ndoa, na wengine wanaishia kuzaa tu watoto na kuwa “single mothers”.
Wale wanaofanikiwa kuolewa kwenye familia za namna hii, huwa wanakuwa na ndoa zenye mateso sana yasiyoisha.
Huwa wanakuwa watu wa kupigwa kwenye ndoa zao au kama hawapigwi basi wanakuwa sio wenye furaha kabisa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.