Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Uchunguzi wa mwili uliofaywa dhidi ya mwili wa mwanablogi wa Kenya Albert Ojwang’, aliyefariki akiwa kizuizini katika Kituo Kikuu cha Polisi umebaini kuwa alivamiwa na kupata majeraha mengi mwilini.
Baada ya kukamilisha uchunguzi wa mwili wake Jumanne Mchunguzi mkuu mwili wa serikali Bernard Midia, alifichua kuwa Ojwang’ hakujigonga ukutani kama ilivyoripotiwa awali katika ripoti ya polisi.
“Tulipochunguza … muundo wa jeraha, hasa kidonda cha kichwani …. inaonyesha kuwa alipigwa na kitu butu kama ukuta ,” alisema.
Midia alisema kwamba katika tukio la mtu kujigonga kwenye ukuta, damu ya mbele juu ya kichwa ingeonekana.
“Lakini damu ambazo tulizipata kichwani…kwenye ngozi ya kichwa zilikuwa zimetengana, ikiwa ni pamoja na usoni, pande za kichwa, na nyuma ya kichwa,” alieleza.
Mchunguzi huyo wamwili, ambaye aliendesha mchakato huo pamoja na mwakilishi wa familia hiyo Mutuma Zambezi alipuuzilia mbali uwezekano wa Ojwang’ kujijeruhi.
Kifo cha Ojwang kilichotokea ndani ya kizuizi katika kituo cha polisi jijini Nairobi kimesababisha ghadhabu miongoni mwa wakenya wengu huku wakitaka wahusika wa kifo chake wachukuliwe hatua za kisheria.
Mamia ya waandamanaji wakiwemo wanaharakati nchini kenya waliandamana kudai haki itendeke.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.