Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maafisa wa Iran wameongeza marufuku ya kutembea kwa mbwa katika miji mingi nchini kote, wakitaja utulivu wa umma na wasiwasi wa afya na usalama.
Marufuku hiyo – ambayo inaakisi amri ya polisi ya 2019 iliyozuia mbwa kutembea katika mji mkuu, Tehran – imeongezwa kwa takriban miji mingine 18 katika wiki iliyopita.
Usafirishaji wa mbwa kwa magari pia umeharamishwa.
Umiliki wa mbwa haupendelewi nchini Iran tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, huku mbwa wakichukuliwa kuwa “najisi” na mamlaka na kama ushawishi wa tamaduni za nchi za Magharibi.
Lakini licha ya hatua hizo umiliki wa mbwa unaongezeka, hasa miongoni mwa vijana, na unatazamwa kama aina ya uasi dhidi ya utawala wa Iran.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.