Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Amua kwa ufasaha unachotaka.
ii. Amini kwamba inawezekana na unastahili kufanikiwa kifedha.
iii. Uwe makini kila siku kufanikisha malengo yako.
iv. Uwe tayari kuwa na nidhamu na kulipa gharama zinazohitajika.
Katika Makala Hii Tutazungumzia hatua ya Tatu
– Uwe Makini Kila Siku Kufanikisha Malengo Yako
Baada ya kujiwekea malengo na kujenga imani na kuona kuwa na wewe unaweza kufanikiwa katika kile ambacho unakifanya;
Hatua inayofuata ni wewe sasa kila siku kuwa makini ili uweze kutumia fursa na watu unaokutana nao ili uweze kufanikiwa katika kupata kiwango cha pesa unachokihitaji.
Unakumbuka katika kitabu cha MALENGO YAKO tulijifunza jinsi mfumo wa ubongo wa RAS unavyofanya kazi? (Kama umesahau basi unaweza kwenda kurudia kujifunza).
Kama hauna kitabu hiki kinachoelezea mbinu 60 wanazotumia watu maarufu kufanikiwa, unaweza kukiagiza kupitia mawasiliano yaliyotolewa kwenye kitabu hiki, hakikisha unakitafuta kitakusaidia sana.
Baada ya kujiwekea malengo na kisha kuamini kwamba inawezekana hatua inayofuata ni wewe kila siku kupanga namna unavyoweza kufanikisha malengo yako.
Katika masomo yanayofuata tutajifunza mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia ili ufanikishe malengo yako ya kifedha kwa kiwango cha juu sana.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.