Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Watu wawili wamefariki baada ya mlipuko kutokea katika mji mkuu wa Uganda Kampala wakati nchi hiyo inaadhimisha Siku ya Mashahidi wa Kikristo.
Tukio hilo lilitokea karibu na moja ya makaburi ambapo maelfu ya waumini wa Kikristo walikuwa wamekusanyika.
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, waathiriwa ni mwanamume na mwanamke waliokuwa wakiendesha pikipiki.
Hata hivyo, Chris Magezi, msemaji wa muda wa jeshi hilo amedai waliofariki ni magaidi ambao walikamatwa wakiwa na vilipuzi.
Usalama umeimarishwa katika eneo la tukio. Hata hivyo mamilioni ya mahujaji wamemiminika mjini Namugongo kusherehekea Siku kuu ya Mashahidi wa Kikristo.
Tukio hilo ambalo ni mojawapo ya mahujaji wengi zaidi wa Kikristo barani Afrika, huwavutia mamilioni ya waumini kila mwaka kuwaenzi mashahidi 45 wa Uganda, Wakatoliki 22 na Waanglikana 23 waliouawa kati ya mwaka 1885 na 1887 kwa amri ya Kabaka Mwanga II wa Buganda kwa kukataa kuacha imani yao.
Nchini Uganda, Juni 3 ni sikukuu ya umma, na maelfu ya watu wanaanza safari ya hija kwa miguu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.