Bill Gates kutoa sehemu kubwa ya utajiri wake wa $200bn kwa Afrika

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bill Gates, ambaye alianzisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft, ndiye mtu wa tano tajiri zaidi duniani
Maelezo ya picha,Bill Gates, ambaye alianzisha kampuni kubwa ya teknolojia ya Microsoft, ndiye mtu wa tano tajiri zaidi duniani

Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates anasema kuwa sehemu kubwa ya mali yake itatumika kuboresha huduma za afya na elimu barani Afrika katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Tajiri huyo mwenye umri wa miaka 69 alisema kuwa “kwa kuibua uwezo wa binadamu kupitia afya na elimu, kila nchi barani Afrika inapaswa kuwa kufikia ustawi wa kijamii”.

Akizungumza katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, pia aliwataka wavumbuzi wachanga Afrika kufikiria jinsi ya kuimarisha teknolojia ya Akili Mnemba (AI) ili kuboresha huduma za afya katika bara hilo.

Mwezi uliopita Gates alitangaza kwamba atatoa 99% ya utajiri wake mkubwa – ambao anatarajia utafikia $200bn (£150bn) – ifikapo 2045, wakati ambapo taasisi yake itakamilisha shughuli zake.

“Hivi majuzi nilitoa ahadi kwamba utajiri wangu utatolewa katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Sehemu kubwa ya ufadhili huo itatumika kukusaidia kutatua changamoto hapa Afrika,” alisema katika hotuba yake katika makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU).

Serikali ya Marekani imepunguza misaada yake kwa mataifa ya Afrika, ikiwa ni pamoja na programu za tiba kwa watu walioambukizwa Virusi Vya UKIMWI na wale walio na UKIMWI, kama sehemu ya sera ya Rais wa Marekani Donald Trump ya “Marekani Kwanza”, na kuibua wasiwasi kuhusu mustakabali wa huduma za afya katika bara hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment