Urusi yathibitisha mashambulizi ya Ukraine kwenye viwanja vya ndege vya kijeshi katika mikoa mitano ya Urusi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

h
Maelezo ya picha,Picha ya kumbukumbu inaonyesha mshambuliaji wa kimkakati wa Tu-95 – Ukraine inasema droni za aina hii zilikuwa miongoni mwa ndege zilizotunguliwa katika mashambulizi ya Jumapili.

Urusi imelaani vikali mashambulizi ya Ukraine dhidi ya viwanja vyake vya ndege ya kijeshi ikiyataja kuwa ”ugaidi”.

Mashambulizi hayo yanakuja wakati wapatanishi wa Urusi na Ukraine wanaelekea Istanbul, Uturuki, kwa duru ya pili ya mazungumzo ya amani siku ya Jumatatu.

Kulingana na Wizara ya ulinzi ya Urusi, viwanja vya ndege ya kijeshi katika mikoa mitano ya Urusi vilishambuliwa na ndege zisizo na rubani.

“Leo, serikali ya Kyiv ilifanya shambulio la kigaidi kwa kutumia ndege zisizo na rubani za FPV dhidi ya viwanja vya ndege katika mikoa ya Murmansk, Irkutsk, Ivanovo, Ryazan na Amur,” Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema katika taarifa.

Wizara hiyo inaripoti kwamba mashambulizi yote katika viwanja vya ndege vya kijeshi katika mikoa ya Ivanovo, Ryazan na Amur yalizuiwa.

Ndege kadhaa ziliwaka moto katika viwanja vya ndege vya kijeshi katika mikoa ya Irkutsk na Murmansk baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani za FPV, Wizara ya Ulinzi ya Urusi inaripoti.

“Moto huo umezimwa. “Hakukuwa na majeruhi kati ya wanajeshi au raia,” jeshi lilisema, na kuongeza kuwa baadhi ya nmashambulizi yamezuiliwa.

Wakati huo huo, kulingana na chanzo cha Idhaa ya BBC Ukraine huko SBU, kkutokana na shambulio hilo kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa wakati wa uvamizi wa Urusi, zaidi ya ndege 40 ziliharibiwa, zikiwemo A-50, Tu-95 na Tu-22 M3.

Wakati huo huo Urusi ilijibu kwa shambulizi la kombora kwenye uwanja wa mazoezi katika mkoa wa Dnipropetrovsk nchini Ukraine siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu 12 na kujeruhi zaidi ya 60. Kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, Mykhailo Drapatiy, aliwasilisha ripoti ya kujiuzulu.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi iliripoti Jumapili jioni kwamba mfumo wa makombora wa Iskander ulipiga kambi ya Wanajeshi wa Ukrain katika eneo la Dnipropetrovsk.

Kulingana na wizara hiyo, kambi ya hema ya brigedi za 158 na 33 tofauti za kikosi cha wanajeshi wa Ukraine kwenye uwanja wa mafunzo wa Novomoskovsk karibu na makazi ya Gvardeyskoye katika mkoa wa Dnepropetrovsk ilipigwa.

Msemaji wa Ground Forces Vitaly Sarantsev aliiambia Idhaa ya BBC Ukraine kwamba kituo cha mafunzo kiko karibu na kijiji cha Cherkasskoye na kwamba janga la sasa sio la kwanza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment