Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki: ‘Hifadhi ya Uranium ya Iran inakua kwa kasi’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

g
Maelezo ya picha,IAEA imetoa matokeo yanayotia wasiwasi kuhusu shughuli za zamani za nyuklia za Iran.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya nyuklia limesema kuwa Iran imepanua zaidi uzalishaji wake wa madini ya uranium iliyorutubishwa sana.

Katika ripoti ya siri iliyoipata BBC, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) lilisema Iran kwa sasa ina zaidi ya kilo 400 za uranium iliyorutubishwa hadi 60%. Hii ni zaidi ya kiwango kinachotumika kwa madhumuni ya kiraia na iko karibu na kiwango cha silaha, na ni sawa na ongezeko la takriban 50% katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kiasi hiki, kikiboreshwa zaidi, kinaweza kutumika kutengeneza takriban silaha 10 za nyuklia, na Iran kwa sasa ndiyo nchi pekee isiyo ya nyuklia inayozalisha kiwango hiki cha uranium.

Iran imeshikilia kwa muda mrefu kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani.

Hata hivyo, IAEA ilisema haiwezi kuthibitisha kama mpango huo bado ulikuwa wa amani.

Iran imezalisha uranium iliyorutubishwa kiasi cha kutosha kwa karibu silaha ya nyuklia kwa mwezi mmoja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, huku kukiwa na mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea kati ya Tehran na Washington.

“Ongezeko kubwa la uzalishaji wa Iran na hifadhi ya uranium iliyorutubishwa sana ni suala la kutia wasiwasi mkubwa,” Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi alisema.

Baada ya ripoti ya IAEA kutolewa, Israel ilitoa taarifa siku ya Jumamosi ikiishutumu Iran kwa “kujitolea kikamilifu kupata silaha za nyuklia.”

Akijibu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alisema Tehran inaziona silaha za nyuklia kama kitu ambacho “hakikubaliki.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment