Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

China inasema Marekani “imekiuka pakubwa” makubaliano yao ya kibiashara na kwamba itachukua hatua kali kutetea maslahi yake.
Wizara ya Biashara ya China ilisema Marekani “imehujumu” makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo huko Geneva mwezi uliopita, ambapo nchi zote mbili zilipunguza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka kwa kila mmoja.
Msemaji huyo aliongeza kuwa hatua za Marekani pia zimekiuka pakubwa maafikiano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya simu mwezi Januari kati ya kiongozi wa China Xi Jinping na Rais Donald Trump.
Maoni hayo yanawadia baada ya Trump kusema siku ya Ijumaa kwamba China “imekiuka kabisa makubaliano yake na sisi”.
Rais wa Marekani hakutoa maelezo lakini Mwakilishi wa Biashara Jamieson Greer baadaye alisema China haikuondoa vikwazo visivyokuwa vya ushuru kama ilivyokubaliwa chini ya makubaliano hayo.
Chini ya mapatano ya kibiashara yaliyofanyika mwezi Mei katika mkutano huko Geneva, Marekani ilipunguza ushuru uliowekwa kwa bidhaa kutoka China kutoka 145% hadi 30%. Ushuru wa kulipiza kisasi wa China kwa bidhaa za Marekani ulipungua kutoka 125% hadi 10%.
Siku ya Jumatatu, Beijing ilisema ukiukaji wa makubaliano ya Marekani ni pamoja na kusitisha uuzaji wa programu za kutengeneza chip za kompyuta kwa makampuni ya China, kuonya dhidi ya kutumia chipu zilizotengenezwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei, na kufuta viza kwa wanafunzi wa China.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa mjini Geneva yaliwashangaza wachambuzi wengi kwani ilionekana kuwa pande hizo mbili ziko mbali sana na masuala mengi ya kibiashara.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.