Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Balozi wa Marekani wa Israel Mike Huckabee amekosoa vikali wito wa Paris wa kulitambua taifa la Palestina, akipendekeza katika taarifa ya kejeli kwamba “ikiwa Ufaransa itadhamiria hivyo, basi itengeneze sehemu ya Riviera ya Ufaransa na kuanzisha taifa la Palestina huko.”
Mwezi huu, Ufaransa kwa ushirikiano na Saudi Arabia, inaongoza kwa pamoja mkutano wa kimataifa katika Umoja wa Mataifa unaolenga kutafuta suluhisho la mataifa hayo mawili, jambo ambalo serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu inapinga.
Paris pia imetangaza kuwa huenda ikatambua taifa la Palestina mwaka huu.
Wakati huo huo, vyanzo vya Palestina vimesema kuwa jeshi la Israel lilifanya msururu wa mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, ambapo walowezi waliwashambulia wakaazi wa Palestina na kusababisha majeraha na uharibifu wa mali.
Duru za habari zimeripoti kuwa wanajeshi wa Israel walivamia mji wa Dura, kusini mwa Hebron, na kuwakamata vijana kadhaa wa Kipalestina wakiwemo wafungwa wa zamani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.