Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Watu Kukulipa Gharama Kwa Wewe Kuonesha Kipaji Chako
ii. Kutengeneza Bidhaa Kupitia Kipaji Chako
iii. Kutumia Jina Lako
iv. Weka Kazi Zako Mtandaoni
v. Kuuza Kipaji Chako Kupitia Wengine/Mfumo
Katika Makala Hii Tutazungumzia Njia ya Kwanza
– Watu Kukulipa Gharama Kwa Wewe Kuonesha Kipaji Chako
Njia ya kwanza ndio maarufu sana kwa watu wengi wenye vipaji.
Mara nyingi kila anayeanza kugeuza kipaji chake kiwe pesa anaanzia hapa.
Lakini hautakiwi kabisa kuishia hapa, huu ni msingi tuu.
Njia hii inamaanisha, ni mabadilishano ya pesa kutoka mikononi mwa watu na wewe kufanya kitu kupitia kipaji chako.
Kutegemeana na aina ya kipaji inaweza kuhusisha kuandaa show fulani ambayo watu wanakuja kuona kipaji chako.
Au kualikwa mahali fulani kwenye tukio ili utumie kipaji chako na watu wakione na ulipwe.
Wakati kipaji kinaanza, watu wengi hufurahia sana njia hii.
Ila baadaye wanakuja kugundua kuwa sio njia ya kudumu sana.
Kwani wanaanza kuchoka sana kwa sababu ya ratiba ngumu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.