Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa Sean ‘Diddy’ Combs’ ametoa ushahidi kwamba msanii huyo wa muziki wa hip-hop alimteka nyara kwa mtutu wa bunduki, kisha kuingia nyumbani kwa rapa Kid Cudi kwa njama ya kumuua.
Capricorn Clark, ambaye alifanya kazi na Bwana Combs kwa zaidi ya muongo mmoja, aliiambia mahakama kwamba mshtakiwa na mlinzi walifika kwenye nyumba yake mwaka 2011 na kumlazimisha kuendesha gari pamoja nao hadi nyumbani kwa Kid Cudi.
“Vaa nguo,” alikumbuka Bw Combs akisema. “Tunaenda kumuua huyu [alitumia neno la matusi].” Pia aliiambia mahakama kwamba Diddy alitishia kumuua katika siku yake ya kwanza kabisa kufanya kazi nyumbani kwake.
Bw Combs, 55, amekana mashtaka ya ulaghai, ulanguzi wa ngono na usafirishaji ili kujihusisha na ukahaba.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.