Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Inakupa Hamasa Ya Maisha (Inner Motivation)
ii. Inakusaidia Kuchagua Vipaumbele Na Kukupa Mwelekeo.
iii. Inakupa Nguvu Ya Kuvumilia.
Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo La Tatu
– Inakupa Nguvu Ya Kuvumilia.
Uvumilivu kwenye maisha ni matokeo ya kile ambacho unakiona mbele yako.
Watu wengi sana wanakata tamaa mapema kwenye Maisha yao kwa sababu hakuna wanachokiona na wanachokitarajia mbele yao.
Musa aliweza kuvumilia kwa sababu kuna kitu alikuwa anakiona moyoni ingawa kwa macho kilikuwa hakionekani (Waebrania 11:27).
Maono ndio yanakupa nguvu za kujitoa kama dhabihu ili tu uweze kukamilisha unachotaka. Yanakupa uwezo wa kukabiliana na maumivu bia kukata tamaa.
Unakuwa tayari kubeba aibu ya muda mfupi kwa sababu unajua kwa hakika kile ambacho unakitaka.
Waebrania 12:2 inasema, “Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu.
Yeye, kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, ALIVUMILIA kifo cha msalaba bila kujali AIBU, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu” Yesu alipata wapi nguvu ya kuvumilia kupigwa, kuchekwa, kutemewa mate, kuvuliwa nguo na kudhalilishwa?
Alikuwa na maono ya ndani yake ambayo ndio yalikuwa yanampa uvumilivu wa hali ya juu sana.
Matokeo ya uvumilivu wake ndio yalimpa nafasi ya kuinuliwa juu na kutimiza alichokuwa anakiona.
Watu wenye maono huwa hawakatishwi tamaa na aibu wanayopitia kwa sasa, huwa wanaamini maono waliyonayo yatakuja kutimia.
Ukiwa na maono hautakata tamaa kwa sababu unaona maono yako yanachelewa, utaendelea mbele kila siku.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.