Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Jeshi la Uganda Jumapili ya wiki hii lilitangaza kusitisha ushirikiano wote wa kiulinzi na Ujerumani, ikimtuhumu balozi wa Berlin, Matthias Schauer kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi huyo.

Msemaji wajeshi la UPDF Chris Magezi, katika taarifa amesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ripoti za kuaminika za kiintelejensia kuwa balozi huyo anajihusisha na vitendo vinavyotishia usalama wa kitaifa.
Licha ya kwamba taarifa hiyo haikuweka wazi vitendo hivyo vinahusisha nini hasa, taarifa hiyo imemtuhumu balozi huyo kwa kushirikiana na makundi ya kisiasa na kijeshi yanayopinga serikali ya Uganda.
Tangazo hilo la jeshi ambalo linazidisha mvutano kati ya Uganda na Ujerumani, inafuatia tangazo lingine la serikali ijumaa iliopita ambayo ilionya kuwa baadhi ya balozi za ulaya zinaunga mkono makundi ya uasi na wasaliti, ujumbe huo ulionekna kumlenga balozi Schauer.
Schauer ambaye amehudumu kama balozi wa Ujerumani nchini Uganda tangu 2020 amekabiliwa na ukosoaji baada ya mkutano wake wa faragha na kaka yake rais Yoweri Museveni ambapo anadaiwa kukosoa tabia ya mtoto wa Museveni na mkuu wa majeshi Muhoozi kainerugaba kwenye mitandao ya kijamii.
Bado haijafahamika namna hatua hiyo itaathiri uhusiano mpana wa kijeshi kati ya Uganda na Ujerumani, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitoa msaada wa vifaa na kiufundi kwa jeshi la Uganda.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.