Mali: Watu wenye silaha washambulia kampuni ya ujenzi ya China

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wanajihadi nchini Mali, mwishoni mwa wiki iliyopita, walitekeleza shambulio kwenye kampuni ya ujenzi nchini China, kwenye jimbo la Kayes, Magharibi mwa nchi hiyo.

Watu hao wenye silaha, walifanikisha mojawapo ya malengo yao, ya kuharibu vifaa vya kampuni hiyo baada ya shambulio hilo.

Shambulio hilo dhidi ya kampuni ya Covec inayojenga barabara kutoka Kayes kwenda Diema, lilipelekea pia wanajihadi hao kuteketeza kwa moto matrektra yanayotumiwa na wajenzi wa barabara hiyo.

Hali hiyo imeacha hali ya wasiwasi kwenye eneo hio, huku wafanyakazi hawa kutoka China wakiachwa kwa hofu, wakati huu ikibainika pia kuwa, wanajihadi hao walilenga kuwateka Wachina kwenye  kampuni.

Hili ni shambulio la pili ndani ya mwezi mmoja, katika jimbo la Kayes, baada ya wanajihadi mapema mwei huu kushambulia mgodi wa madini, unaomilikiwa na wawekezaji kutoka China.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment