Korea Kaskazini yamkamata afisa mkuu kwa kushindwa kuzindua meli ya kivita

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Korea Kaskazini imemkamata afisa wa nne kutokana na kushindwa kuzinduliwa kwa meli mpya ya kivita jambo ambalo limemkasirisha kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un.

Ri Hyong-son, naibu mkurugenzi wa Idara ya viwanda vya silaha wa Chama tawala, “alihusika kwa kiasi kikubwa kwa matokeo hayo”, shirika la habari la serikali KCNA lilisema Jumatatu.

Meli hiyo ilikuwa imeharibika sehemu yake ya ndani, katika kile Kim alichoeleza kama “kitendo cha uhalifu” ambacho “kiliharibu sana heshima na sifa ya [nchi]” hiyo.

Chombo hicho kinarekebishwa chini ya mwongozo wa kikundi cha wataalam, KCNA alisema.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment