Vita vya Ukraine: Urusi yaushambulia mji mkuu wa Ukraine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

f

Watu 15 wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kuharibiwa baada ya Urusi kushambulia mji wa Kyiv kwa makombora na ndege zisizokuwa na rubani usiku wa kuamkia Jumamosi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kuwa ulikuwa ‘usiku mbaya’ kwa taifa hilo.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii, Zelensky ameitaka jamii ya kimataifa kuiwekea Urusi shinikizo kupitia vikwazo zaidi ili ikubali kusitisha mapigano.

Maafisa wa usalama mjini Kyiv wanasema kuwa mashambulizi hayo yalitokea katika wilaya sita, huku eneo la Obolon kaskazini magharibi mwa Kyiv ikiathirika vibaya.

Siku ya Ijumaa, mataifa hayo mawili yalishiriki katika zoezi kubwa la kubadilishana wafungwa, huku rais wa Marekani Donald Trump akisema hii ni hatua nzuri katika juhudi za kuleta amani kati ya pande mbili.

Hata hivyo, Moscow na Kyiv zimelaumiana kwa kutokuwa na nia ya kumaliza vita hivyo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment