Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Chanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha, Boniface Mwangi aliachiliwa kutoka kizuizini nchini Tanzania na kuachwa kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wa Lungalunga- Marekani inatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa haraka na kamili juu ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Tanzania baada yakushikiliwa kwa wanaharakati wa Kwenya na Uganda- Boniface Mwangi na Agather Atuhaire, ambao sasa wameachiliwa.Mwanaharakati Boniface Mwangi na Agather Atuhaire wa Uganda walizuiliwa nchini Tanzania mapema wiki hii nchini Tanzania, ambao walikuwa wameenda kuhudhuria kesi ya kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu.Kupitia ujumbe wakwe kwenye mtandao wa X, Wizara ya mambo ya nje ya marekani , idara inayohusika na masuala ya Afrika imesema: ‘’ Marekani ina wasiwasi mkubwa na ripoti za unyanyasaji nchini Tanzania kwa wanaharakati wawili wa Afrika Mashariki – mwanaharakati wa Uganda Agather Atuhaire na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi. Atuhaire alitambuliwa na @StateDept [Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani] mnamo 2024 kama Mshindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wa Ujasiri’’Ujumbe huo umeendelea kusema kuwa :‘’Tunatoa wito wa uchunguzi wa haraka na kamili juu ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Tunahimiza nchi zote katika eneo hili kuwawajibisha wale waliohusika na kukiuka haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mateso.’’Mwangi aliachiliwa huru siku ya Alhamisi baada ya Kenya kutoa wito kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua ya “haraka na bila kuchelewa” ili kuwezesha ufikiwaji wa kibalozi au kuachiliwa kwa Mwangi, kwa mujibu wa sheria na kanuni za kimataifa kidiplomasia.Mwangi ambaye aliachiliwa na kuachwa kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wa lungalunga alidai kuwa aliteswa alipokuwa Tanzania.
Chanzo cha picha,AFP via Getty ImagesMaelezo ya picha,Agather Atuhaire alidai kuteswa akiwa kizuizini Tanzania - Patience Atuhayire, ambaye ni mwanaharakati wa Uganda ambaye alikamatwa na kushikiliwa kwa siku kadhaa nchini pia nchini Tanzania aliachiliwa na kupatikana kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili akiwa na “dalili za mateso,” shirika lake la kutetea haki za binadamu linasema. Mwangi: Mfahamu mwanaharakati wa Kenya mwenye utataMwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi aachiwa huru TanzaniaMtandao wa X na harakati za mapambano mtandaoni TanzaniaMshirikishe mwenzako, Mwangi & Atuhaire: Marekani yataka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Tanzania
- Muungano wa Ulaya wataka ‘heshima’ baada ya Trump kutishia ushuru wa 50%.
EPAMaelezo ya picha,Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya (EU), Maros Sefcovic ameonya kwamba Ulaya “wako tayari kutetea maslahi yetu”Mkuu wa biashara wa Umoja wa Ulaya alisema jumuiya hiyo yenye wanachama 27 imejitolea kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani kwa kuzingatia “heshima” na sio “vitisho”.Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kutoza ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa zote zinazotumwa Marekani kutoka Umoja wa Ulaya.”EU inajihusisha kikamilifu, imejitolea kufikia makubaliano ambayo yatawafaa wote wawili,” Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Maros Sefcovic alisema baada ya mazungumzo na Muwakilishi wa masuala ya Biashara wa Marekani Jamieson Greer na Waziri wa Biashara Howard Lutnick.”Biashara ya EU na Marekani hailinganishwi na lazima iongozwe na kuheshimiana, si vitisho. Tuko tayari kutetea maslahi yetu.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.