Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Miaka mingi iliyopita nilikutana na mtu ambaye nilikuwa nasikia sana habari zake mbaya…
…na alikuwa akizungumzwa sana ubaya wake na mtu mwingine ambaye nilikuwa namfahamu.
Ukweli ni kuwa hata mtazamo wangu juu yake uliathiriwa sana na ulikuwa “negative” mno…
…hata kama nilikuwa simjui sana na kuwa karibu naye lakini tayari niliona ndani yangu simkubali…
…na nilishahitimisha kuwa ni mtu mwenye sifa zote mbaya nilizokuwa nazisikia.
Siku niliyokutana naye alikuwa amekuja kuniomba ushauri.
Nilipokutana naye hakujua kuwa nina taarifa zake nyingi sana nilizoambiwa…
…na watu ambazo zilinifanya hata kabla hajasema niwe nimeshamuhukumu na kumuona si mtu sahihi…
…lakini nilimpa nafasi ya kumsikiliza.
Alipoanza kuongea nilishangaa sana, katika mambo niliyoambiwa takribani 98% hayakuwa kweli.
Na cha ajabu zaidi alikuwa anapitia wakati mgumu sana…
…na alikuwa na vita nyingi sana katika maisha yake ambazo watu wengi sana walikuwa hawajui kabisa.
Alinieleza kuhusu maumivu yake…
Alinieleza kuhusu changamoto zake…
Alinieleza alivyobakia peke yake na kila mtu amemkimbia…
Alinieleza jinsi ambavyo hakuna mtu wa kumsikiliza…
Alinieleza ambavyo amekata tamaa kwa sababu ya maneno ya kuchoma moyo ya uongo ambayo kila siku yanasemwa juu yake n.k
Nilishikwa na huzuni Moyoni, nilimuomba msamaha:
Nilijifunza kuwa kabla HAUJAMCHUKIA mtu tafuta SABABU ya KUMPENDA.
Kabla HAUJAMSEMA VIBAYA tafuta SIFA ZAKE NZURI.
Nilijifunza kuwa kuna watu WANATESEKA na MANENO MABAYA…
…ambayo wewe Unayasema kwa KUJIFURAHISHA wenzako YANAWATESA.
USIMUHUKUMU MTU bila KUPATA NAFASI YA KUMSIKILIZA.
USIMCHUKIE mtu kwa MANENO YA WENGINE.
Kuna mtu ANAHITAJI kupona leo kwa UPENDO wako.
USIRUHUSU CHUKI na MANENO YAKO yawe chanzo cha YEYE KUKATA TAMAA.
Tafuta Mtu wa KUMGAWIA FURAHA na TUMAINI kwa MANENO YAKO na sio KUSABABISHA HUZUNI.
Kuna mengi unayoweza kuyaamini yakawa si kweli.
UWE CHANZO CHA FURAHA KWA MTU MWINGINE LEO.
USIHUKUMU kabla HAUJASIKILIZA.
USIAMINI kabla HAUJATHIBITISHA.
USITENGENEZE MSIMAMO kwa KUSIKIA kwa WENGINE TU.
GAWA FURAHA LEO!!
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.