Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mwanaharakati Agather Atuhaire, ambaye alikuwa akishikiliwa nchini Tanzania, amepatikana akiwa ametupwa karibu na mpaka wa Mutukula wa Uganda usiku, familia yake na marafiki zake wamethibitisha. NTV imeripoti.
Mwanaharakati Agather Atuhaire wa Uganda alizuiliwa nchini Tanzania pamoja na mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi mapema wiki hii.
Wanaharakati hao walikuwa wameenda kuhudhuria kesi ya kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wiki hii alitoa onyo kali kwa wanaharakati kutoka nchi jirani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, akisisitiza kuwa taifa hilo haliwezi kuwa “shamba la bibi” ambapo kila mtu anaingia na kufanya apendavyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa toleo jipya la Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024), Rais Samia alisema kuna mwenendo unaoibuka wa baadhi ya wanaharakati kuvuka mipaka na kuingilia masuala ya ndani ya nchi, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa.
“Tusiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mtitiriko au mwenendo wa wanaharakati ndani ya region (kanda) yetu hii, kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku,” alisema Rais Samia.
Kauli hiyo aliitoa siku moja baada ya wakili mashuhuri wa Kenya na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, pamoja na Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga kuzuiwa kuingia nchini Tanzania.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.