JIZUIE NA HATARI YA RAFIKI YAKO KUANZISHA URAFIKI NA MAADUI ZAKO

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Stori ya Lumumba na Mobutu.

Baada ya majadiliano ya kwanza kuhusiana na uhuru wa Kongo (DRC) yaliyofanyika Brussels, makubaliano ya awali yalifikiwa kuwa wapewe uhuru wao tarehe 30 June, 1960.

Patrice Lumumba aliyekuwa akiongoza mazungumzo hayo alilazimika kuanza safari ya kurudi Congo ili kuanza maandalizi wakati majadiliano mengine yakiendelea.

Baada ya makubaliano ya kisiasa, yalifuata makubaliano ya kiuchumi kuhusiana na rasilimali za Congo.

Lumumba alimuamini rafiki yake, Joe Mobutu kuongoza round ya pili ya majadiliano. Ukiacha tu ukweli kwamba “walipigwa” kwenye majadiliano kutokana na uzoefu wa watu waliokuwa upande wao na upande wa ubelgiji(Hadi wakati huu ni wacongo 17 tu ndio walikuwa wana shahada).

Jambo lingine ambalo Lumumba alikuwa halijui ni kuwa “maagent” wa CIA na Soviet walikuwa tayari wako Brusells wakizengea viongozi wa Congo waliobakia.

Walifanikiwa kumpandikizia chuki Mobutu dhidi ya rafiki yake Lumumba, na Chief wa CIA Leopoldville(Kinshasa) Larry Delvin, alimuingiza katika orodha ya malipo rasmi.

Rafiki yake wa karibu aliywahi kumfanya “Private Secretary” wake akiwa Waziri Mkuu, ndiye alishirikiana na adui zake.

Sio tu aliagiza kukamwatwa kwa Lumumba , bali aliagiza auwawe kwa kupigwa risasi , mwili kukatwa na msumeno na siku ya pili aliagiza wafukue mwili na uyeyushwe kwa tindikali ili kupoteza ushahidi.

Mungu akupe macho kujua pale rafiki yako anapoanza kujenga urafiki na adui zako.

Ukiona dalili usipuuzie!

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment